Chapa ya Impact

    Chapa ya toleo la Impact ni sehemu ya Global Health Unit ya Sanofi (GHU) shirika la kibiasha ya kijamii la Sanofi.

    Bidhaa zenye chapa ya Impact ni sawa na bidhaa asili za Sanofi ila tu kwa jina tofauti. Bidhaa zenye chapa ya Impact haziwezi kutolewa kijeneriki kwa vyovyote vile.

    Lengo la Sanofi GHU's ni kufanya dawa za thamani bora zipatikane kwa ajili ya wagonjwa walio katika katika nchi zilizoteuliwa zenye mapato ya chini na ya kati. Nchi zingine zitadumisha majina ya chapa asili.

    Kabadilisha majina kwa ajili ya Nchi za Mapato ya Chini na Kati (LMCs) kunatuwezesha kusambaza bidhaa vivyo hivyo kwa bei ya chini bila kuingia kwenye hatari ya kuendesha biashara sambamba. Lengo ni kuhakikisha kuwa wagonjwa katika hizo LMCs wanaweza kupata dawa za matibabu kwa bei nafuu.

    Viwanda vyetu vya uzalishaji vitatengeneza aina za kipekee za Impact kwa LMCs badala ya aina kadhaa zinazo sambazwa kwa sasa. Inaturuhusu kuzidisha viwango vya uzalishaji na kupunguza gharama za uzalishaji. Uzidishaji huu utasababisha bei nafuu kwa wagonjwa. 

    Bidhaa za Impact ni sawa kabisa na chapa asili za bidhaa hivyo.

    • Vina ubora sawa kabisa
    • Vinazalishwa katika kiwanda kimoja na matoleo ya chapa asili
    • Tofauti pekee ni jina na ufungaji: ufungaji wa kipekee ambao umewekwa msimbo wa QR na ufikio wa vijikaratasi kwa lugha mbalimbali za maeneo husika.

Kukadiria bei na uzalishaji

    Kwa sababu tunaboresha gharama za mkondo usambazaji, bidhaa vya chapa ya Impact vinaweza kutolewa kwa bei nafuu kushinda chapa za matoleo ya asili.

    Jibu fupi ni la. Bidhaaa za Impact zinatengenezwa katika viwanda vilevile ambavyo bidhaa za asili za Sanofi zinatengenezewa. Hii ina maana kuwa ziko chini ya thamani moja ya udhibiti na sheria za mchaka.

    Michakato yetu ya thamani ya ubora ngumu sana, mwanafamasia wetu anayewajibika atadhibiti na kuwachilia bidhaa za chapa ya  Impact kwa mujibu wa vigezo sawa vya utengenezaji kama vya bidhaa za asili.

    Wakati mtambo wetu wa uzalishaji unatengeneza bidhaa, hakuna tofauti hadi hatua za mwisho kabisa za mchakato wa ufungaji: mtambo utafunga bidhaa kwenye maboksi kwa chapa ya Impact. Kwa maneno mengine hakuna tofauti kabisa katika ubora na bidhaa hizo ni moja.

    Kuzusha bei kunaweza kusababisha hatari ya biashara kinzani katika nchi jirani, jambo linalomaanisha kuwa wateja hawatapata manufaa kutokana na bei nafuu na hatutaweza kufikia idadi ya watu walio na uhitaji wa hali ya juu.

    Lengo la GHU ya Sanofi ni kuweza kudumu na kutoa bei nafuu zaidi kwa wagonjwa. Bei zinazotolewa zinaambatana na gharama ya bidhaa jambo linalowezesha GHU ya Sanofi kusambaza kwa bei za nafuu.

    Hata hivyo,gharama zetu za bidhaa pia zinategemea bei za malighafi, bei za nishati, mishahara ya wafanyakazi na udhibiti wa kimazingira. Hili lina maana kuwa bei zinaweza kubadilika, kulingana na vipengele hivi. Lakini thamani itabaki ileile kila mara.

    Bei zitakuwa tofauti kwa sababu mkondo wa usambazaji ni tofauti.

    Katika soko la umma, kwa ajili viwango muhimu (kwa mfano zabuni za Wizara ya Afya) mkondo wa usambazaji utakuwa mfupi (idadi ndogo ya madalali).

    Katika soko la kibinafsi, mkondo wa usambazaji unaweza kuwa mrefu (wasambazaji, wauzaji wa jumla, na wanafamasia). Kwa hivyo bei zitakuwa ghali.

    Pia tutasambaza bidhaa hadi kwa Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserekali (NGOs), yanayoweza kutoa dawa kwa wagonjwa bila malipo.

    Kabla ya kuzindua bidhaa za Impact, tutathibitisha uwezo wa mtambo wa uzalishaji changamoto. Ni baaada tu ya kiwanda kuthibitisha uwezo wa kutengeneza bidhaa kwa ajili ya mataifa ya GHU ndipo tutafanya uzinduzi wa bidhaa.

    Bidhaa ambavyo tumechagua kuweka chapa chini ya jina la Impact pia zilichaguliwa kwa sababu tunajua tunaweza kudumisha uzalishaji katika nchi zote za GHU. 

    GHU ya Sanofi iliwekeza rasilimali muhimu ili kuzindua  chapa Impact ili wagonjwa wafikio bidhaa zetu, vilivyo na ubora uleule lakini kwa bei nafuu. Hatungeweza kuwekeza kwa shughuli hii ikiwa hatungekuwa na uhakika wa kudumisha uzalishaji.

Sako na ubalishaji wa chapa

    Tulipata ya kwamba katika nchi zingine wagonjwa hawapati dawa yenye thamani bora kwa sababu ya bei ghali ima kwa sababu ya ugumu wa kupatikana kwa dawa kutokana na matatizo ya mkondo wa usambazaji. 

    Ili kushinda hili, tunajitolea kwa mkakati wa biashara ya kijamii unaosaidia kupunguza changamoto hizi katika nchi tunazofanya kazi.

    Hiyo inategemea na hali ya kila nchi.

    Ikiwa chapa ya asili tayari imesajiliwa katika nchi na bidhaa za Impact zimesajiliwa kabla ya muda kumalizika, chapa zote mbili zitakuweko. Hata hivyo, baada ya muda upatikananji wa chapa asili utapungua na upatikanaji wa chapa ya Impact kuongezeka.

    Nchi tunazoendesha shughuli katika mabara yote 5 inaana kuwa idadi kubwa ya wagonjwa wanaongea lugha nyingi.  Si wagonjwa wote wanaosoma Kiingereza. Ndiyo sababu, tumebuni mbinu ya kipekee ya ufungaji ambayo ina msimbo wa QR yenye vikjikaratasi vilivyo katika lugha mbalimbali.

    Unaposkani msimbo wa QR unapata kufikia tovuti zinazokudokezea kufungua kijikaratasi cha kielektroniki ima kwa Kihispania, Kiarabu, Kirusi, Kilao, Kikhmer, Kiburma, Kipashto au Kiswahili.  Tunaweza kuongeza lugha zingine. 

Je, hujapata jibu lako?  

Usijali tuko hapa kukusaidia! Tutafikie kisha tuongee. 

MAT-GLB-2304595
DOP: Oktoba 2023