Jinsi tunavyo fanya mabadiliko
Tukiwa tumeambatana na malengo Endelevu ya 3, 8, na 17, ya Umoja wa Mataifa tunafanya juhudi kuleta mabadiliko katika kuzikabili changamoto za afya-msingi katika Nchi za Mapato ya Kiwango cha Chini na Kati. Juhudi zetu zinalenga maeneo yafuatayo:

Kuboresha matokeo kwa wateja
Kutoa matibabu kwa bei zinazoweza kufikiwa na kushirikiana kubuni mipango na umma na washirika wa NGO.

Kujenga ushikiano wa kuleta mabadiliko katika sekta mbalimbali
Kufadhili mipango pamoja na umma na washirika wa NGO na kusaidia biashara za kijamii, ikiwemo usawa wa uwekezaji.

Kuimarisha mifumo ya kiafya
Kutoa misaada isiyo ya kifedha, usaidizi wa kiufundi na ushauri kwa njia ya mazungumzo na wafanyakazi.
Pata maudhui yanayo kufaa
Chapa ya Impact
Chapa ya toleo la Impact inalenga huduma ya afya kuhusu magonjwa yasiyoambukizwa (NCDs), kama vile ugonjwa wa moyo, saratani, kisukari, katika nchi zilizoteuliwa tunakoendesha shughuli kote duniani.

Changamoo za NCDs
Kila mwaka, watu milioni 17 wanakufa kutokana na NCD kabla ya kufika umri miaka 70 na 86% ya vifo hivi hutokea katika Nchi za Mapato ya Kiwango cha Chini na Kati.1
- Matibabu ya NCD ni marefu na ni ya bei ghali na yanachangia umaskini kutokana na gharama za kiasi kikubwa za kimatibabu na matumizi ya hali ya juu kutoka mfukoni.
- Watu walio katika nchi za mapato ya kiwango cha chini na kati wanao ufikio finyu kwa huduma fanisi za afya na zenye usawa, jambo linalochelewesha ugunduzi wa magonjwa na hatari ya vifo vingi vya mapema.

Jinsi tunavyoshughulikia changamoto hizi
Ili kushughulikia changamoto za NCDs katika nchi zinazokua, Global Health Unit ya Sanofi imebuni suluhisho linaloweza kufikiwa ili kuleta sokoni viwango kadhaa vya huduma za matibabu ya NCD chini chapa ya jina la Impact (INN + Impact).
Kutolewa kwa huduma mbalimbali za Impact na nchi za GHU kutachukua nafasi ya chapa zinazofanana za Sanofi zilizokuweko awali kwa ajili ya magonjwa haya.

Ubora uleule, jina tofauti
Bila kupunguza ubora, jambo la pekee linalobadilika kutoka kwa bidhaa za chapa za Sanofi na kuchukua chapa ya Impact ni jina na ufungaji.
- Kutoa bei za kumudu kwa dawa hizi, hivyo kutoa ubora wa kuwafikia wagonjwa wengi
- Kutumia kifungio kimoja cha kipekee katika nchi zote katika nchi tunazoendesha shughuli ili kusaidia katika kukinga biashara kinzani
Kuzindua Impact badala ya chapa asili ya Sanofi kunatusaidia:
Kwa taarifa zaidi kuhusu badiliko hili, tembelea eneo letu la FAQ


Jon Fairest
Kiongozi wa Global Health Unit, Sanofi
"Tunafanya kazi kuboresha ufikiaji wa dawa muhimu huku tukikuza huduma ya afya yenye thamani bora na endelevu kwa ajili ya watu wa nchi maskini. Ni muhimu kuwa tunafanya kazi na washirika ulimwenguni, kanda na maeneo husika, ili kuleta mabadiliko ya mageuzi na ya kudumu. Kwa kuunda mipango kabambe ya masuala ya afya ambayo imekumbatiwa katika jamii wanazohudumia, tunayo fursa kubwa ya kuboresha huduma na kuunda dunia stahimilivu zaidi"
Jinsi tunavyofanya kazi
Gundua kiini cha tunayofanya ili kushughulikia changamoto za NCDs na kuboresha huduma kwa ajili ya wagonjwa.
-1.jpg/jcr:content/MicrosoftTeams-image%20(18)%201.jpg 400w, /.imaging/webp/sanofi-platform/img-w500/dam/impact-sanofi-tz/what-is-impact-/MicrosoftTeams-image-(18)-1.jpg/jcr:content/MicrosoftTeams-image%20(18)%201.jpg 500w, /.imaging/webp/sanofi-platform/img-w600/dam/impact-sanofi-tz/what-is-impact-/MicrosoftTeams-image-(18)-1.jpg/jcr:content/MicrosoftTeams-image%20(18)%201.jpg 600w, /.imaging/webp/sanofi-platform/img-w700/dam/impact-sanofi-tz/what-is-impact-/MicrosoftTeams-image-(18)-1.jpg/jcr:content/MicrosoftTeams-image%20(18)%201.jpg 700w, /.imaging/webp/sanofi-platform/img-w800/dam/impact-sanofi-tz/what-is-impact-/MicrosoftTeams-image-(18)-1.jpg/jcr:content/MicrosoftTeams-image%20(18)%201.jpg 800w, /.imaging/webp/sanofi-platform/img-w900/dam/impact-sanofi-tz/what-is-impact-/MicrosoftTeams-image-(18)-1.jpg/jcr:content/MicrosoftTeams-image%20(18)%201.jpg 900w, /.imaging/webp/sanofi-platform/img-w1200/dam/impact-sanofi-tz/what-is-impact-/MicrosoftTeams-image-(18)-1.jpg/jcr:content/MicrosoftTeams-image%20(18)%201.jpg 1200w)
Maadili na Kazi ya Impact Fund ni
Muktadha
Katika hali ambayo magonjwa yasiyo ya kuambukiza (NCDs) yanaongezeka, kupata huduma bora za afya bado hakutoshi na kwa kiasi kikubwa hakutoshi kwa watu bilioni 6.5 katika nchi za kipato cha kiwango cha chini na cha kati (low- and middle-income countries, LMICs). Wabunifu wanagundua teknolojia mpya na mazoea ya kibiashara yanayoshughulikia changamoto zinazojulikana za mifumo ya afya, ikiwemo upungufu wa ugavi, ufuatiliaji mdogo wa dawa, kutomudu gharama ya huduma, mafunzo ya kutosha ya wafanyakazi wa matibabu, kutofikiwa vya kutosha, ukosefu wa tabia za kuzuia na mengine.
Maadili
Tunaamini kwamba ni jukumu letu kuleta utofauti katika maisha ya wahitaji zaidi na kusaidia kuandaa mabadiliko endelevu kwa kuandaa ufikio sawa wa dawa na mipango inayoimarisha mifumo ya mazingira ya huduma ya afya.
Kazi
Impact Fund ya Sanofi inaunga mkono uboreshaji wa ubia endelevu wa ndani unaotoa masuluhisho bunifu na yaliyoundwa kwa ajili ya changamoto za ndani kwa kuboresha ufikio wa matibabu na huduma ya ubora wa bei kwa wagonjwa ambao hawajahudumiwa vya kutosha, kuchanganya uvumbuzi wa kidijitali na mbinu za uwasilisho hasa katika maeneo husika. Kwa kutoa ufadhili jumuishi wa kibiashara na misaada ya kiufundi, hazina hii inasaidia kushughulikia mapengo ya ufadhili katika huduma za afya ambayo yanaendelea kudumu katika nchi nyingi za mapato ya kiwango cha chini na kati.
Mbinu ya Uwekezaji wa Impact Fund
Mtazamo wa Impact kwa mahitaji ya juu ambayo hayajatimizwa
-
Uwekezaji katika makampuni yaliyo kwenye hatua za awali na ukuaji.
-
Mtazamo wa kipekee kwa wagonjwa ambao hawajahudumiwa vya kutosha na nchi za kipato cha kiwango cha chini (nchi 40 zinaenea katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara na Kusini-Mashariki mwa Asia).
-
Kulenga mzigo wa magonjwa yasiyoambukizwa.
-
Kusizitiza kuhusu uwezo wa kuimarisha na kuzidisha mtindo wa kibiashara.
Vipengele vya uwekezaji: “Impact first” mtaji wa mgonjwa, na vyombo vilivyobuniwa
-
Hazina ya €25M inayotoa usawa wa €0.5M-5M, usawa wa mikopo huria na uwekezaji mseto wa moja kwa moja.
-
Kuwekeza kama wanahisa wachache.
-
Kuhifadhi mtaji, kwa Impact first.
-
Upeo wa uwekezaji wa yapata miaka 10 ili kuunda ushirikiano wa muda mrefu na makampuni ya yaliyoko.
-
Uwezo wa kuvutia ufadhili wa kichocheo.
Zaidi ya hayo: Beyond capital, mshirika wa kimkakati wa muda mrefu
-
Kufanya kazi kwa ushirikiano na usimamizi kuhusu usaidizi katika mradi wa kiufundi kabla na baada ya uwekezaji na uzidishaji.
-
Kutumia uwezo wa ndani wa Sanofi, ufikiaji wa wataalam na mitandao.
-
Kuchunguza ushirikiano na Sanofi Global Health kupitia upatikanaji wa bidhaa mbalimbali za bei nafuu za Impact®, ruzuku za kuondoa hatari ya uvumbuzi, ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi na/au utetezi.
Ikiwa unahitaji taarifa yoyote ya ziada kuhusu GHU ya Sanofi na Impact Fund, tafadhali tuma baruapepe kwa: Sanofi_Global_Health@sanofi.com
Mawekezo yetu
Katika nchi nyingi za mapato ya kiwango cha chini na kati, kutofikia huduma za wataalam wa huduma ya afya mara nyingi husababisha kutegemea wanafamasia pakubwa kwa kupata haduma-msingi za afya. Tumeshirikiana na SwipeRx, jukwaa kuu la kiteknolojia linalosaidia famasia ndogo za mitaa kuboresha upatikanaji na uwezo wa kumudu dawa na huduma kwa wagonjwa kote katika Kusinimashariki mwa Asia. SwipeRx ni jukwaa moja linalowezesha elimu na ushirikiano, eneo moja kuu la kufanya ununuzi, ufadhili wa kifedha, na masuluhisho ya kimkakati kwa ajili ya wanafamasia.
Moja kati ya wanafamasia watatu katika Kusinimasharika mwa Asia wanatumia SwipeRx. Mkataba huu, unaojumuisha mawekezo ya kifedha na kusaidia wajibu wa kibiashara ya Sanofi, itasaidia uwezo wa SwipeRx’s kuimarisha na kukuza mfumo wake wa kibiashara katika nchi za mapato ya kiwango cha chini wanachama wa Global Health Unit, kama vile Cambodia.
Je una swali
au unahitaji msaada? 
Pata majibu ya maswali ya kila mara katika eneo letu la Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi (FAQ). Labda swali lako limewahi kuulizwa tayari. Ikiwa hutapata jibu lako, unakaribishwa kila mara kuwasiliana nasi.
Marejeleo
- WHO. https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/noncommunicable-diseases, Ilitembelewa mara ya mwisho Julai 2023.
MAT-GLB-2304595
DOP: Oktoba 2023