Sababu Kuu ya Vifo

Magonjwa yasiyoambukizwa (Noncommunicable diseases, NCDs) kama ugonjwa moyo, saratani, na kisukari, ni sababu kuu za vifo duniani. Kila mwaka, watu milioni 41 wanakufa kutokana na NCDs, milioni 15 kati ya umri wa 30 na 69. Licha ya masuluhisho mengi ambayo yamethibitishwa, maendeleo yamekuwa polepole na yasiyo dhabiti.

Uchambuzi wa hali ya Magonjwa Yasiyoambukizwa katika Nchi Zilizo na Mapato ya Kiwango cha Chin na cha Kati

Ripoti hii kuhusu Uchambuzi wa hali ya Magonjwa Yasiyoambukizwa katika Nchi Zilizo na Mapato ya Kiwango cha Chin na cha Kati (Low and Middle Income Countries, LMIC) inayotolewa na Path.Org, inatoa mhutasari wa mazingira ya NCD, malezo ya matokeo msingi, na mapendekezo kwa ajili ya hatua za siku zijazo kwa kutumia wahusika wasio wa kiserekali.

Mandhari haya yanatazamwa kwa mtazamo wa miundo ya mfumo wa Shirika afya Afya Duniani (World Health Organization’s,WHO’s) ambao unafafanua vigezo vikuu sita vya ujenzi, ikiwemo:

  • Kutoa huduma
  • Jopokazi ya afya
  • Taarifa
  • Bidhaa za matibabu, chanjo, na teknolojia
  • Ufadhili wa kifedha
  • Uongozi na usimamizi.

Thathmini hii ipo kwa majira mwafaka nchi zinapo andaa mchakato wa Usimamizi wa Afya ya Jumla Universal Health Coverage, UHC). Katika nchi nyingi, NCDs kama vile shinikizo la damu, kisukari, matatizo ya kiakili, na satani yametajwa kama kiungo muhimu cha kutoa huduma za vituoni na haduma za kinga ambazo zinapasa kuongezwa nguvu ili kuafikia UHC. Shinikizo la Damu (Hypertension, HTN) na kisukari yalichaguliwa kwa malengo kuweka mandhari haya wanapoongoza NCDs miongoni mwa NCDs nne kuu.

Ingawa manthari haya yalitazamwa kwa mtazamo vigezo vya ujenzi vya mifumo ya afya vya WHO matokeo na mapendekezo yanawasilishwa kote katika kwenye nguzo nne: Ufikiaji, Mtindo wa Miunganisho ya Huduma, Juhudi Endelevu — kupanga taarifa na uchambuzi kwa mtazamo unaolenga kutoa kipaumbele kwa nafasi wazi na fursa za kuingilia kati na ushirikiano hasa kwa wahusika wasio wa kiserekali. Kupitia kwa kushiriki mafunzo kutoka kwa uchambuzi huu wa hali pamoja na jamii ya ulimwenguni, lengo letu ni kudhihirisha mahitaji yaliyopo ambayo hayajashughulikiwa katika mazingira ya nchi za Mapato ya Kiwango Cha Chini Na Kati (Low and Middle Income Country, LMIC) na palipo na fursa za muungano na ushirikiano ili kushughulikia haya. 

MAT-GLB-2304595
DOP: Oktoba 2023