Kuanzia Clexane® Lovenox® hadi Enoxaparin Sodium Impact®
Enoxaparin Sodium Impact® ni bidhaa moja na ubora ule mmoja na Clexane®, ila kwa jina tofauti tu. Mbona jina liwe tofauti? Kwa sababu hili linatusaidia kutoa dawa hii katika nchi yako kwa bei nafuu zaidi. Soma zaidi kuhusu ni kwa nini bei ya bidhaa hii inabadilika katika FAQ.
Enoxaparin Sodium Impact uzalishaji wa kwanza katika Maisons-Alfort
Rasilimali kwa ajili ya wagonjwa
Wasaidie wagonjwa wako kwa raslimali zinazohusu Enoxaparin Sodium Impact® na jinsi ya kutoa matibabu yao.
Kijikaratasi cha taarifa ya mgonjwa
Wape wagonjwa wako muhtasari wa matibabu yao kwa dawa ya Enoxaparin Sodium Impact. Kijikaratasi hiki kinapatikana katika lugha nyingi.
Je una swali
au unahitaji msaada? 
Pata majibu ya maswali ya kila mara katika eneo letu la Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi (FAQ). Labda swali lako limewahi kuulizwa tayari. Ikiwa hutapata jibu lako, unakaribishwa kila mara kuwasiliana nasi.
Kukiwa na malalamiko kuhusu ubora wa bidhaa kushuku udanganyifu, bandia au bidhaa visivyotumika ilivyokusudiwa, tafadhali andikia Quality.PartnerMarketsAfrica@sanofi.com. Tafadhali shiriki nasi maelezo ya sampuli au picha ya dawa kasoro au bidhaa kasoro, na taarifa kuhusu jina la bidhaa hiyo, nambari ya toleo, tarehe ya mwisho wa matumizi na idadi.
Tafadhali pia wasilisha kwa Sanofi (Quality.PartnerMarketsAfrica@sanofi.com) taarifa yoyote kuhusu bidhaa zinazoshukiwa kuwa za udanganyifu, bandia au zinazotumika isivyokusudiwa.
Lugha ya Kiingereza ikiwezekana inapendekezwa kwa ajili ya mchakato wa haraka.
Ikiwa una wasiwasi kuhusu afya yako, hali yako, au athari zozote za kimatibabu unazokuwa unashuhudia, zungumza na daktari au mwanafamasia wako. Unaweza kutoa taarifa kuhusu athari zozote za kimatibabu kwa Mamlaka ya Afya au moja kwa moja kwa sanofi kupitia jukwaa letu la kimtandao ae.reporting.sanofi. Kwa kuripoti athari za kimatibabu unaweza kusaidia kwa kutoa taarifa zaidi kuhusu usalama wa dawa hii.
Rejeo
- Enoxaparin Sodium Impact® SmPC.
MAT-GLB-2304595
DOP: Oktoba 2023