
Jinsi tunavyo fanya mabadiliko
Tukiwa tumeambatana na malengo Endelevu ya 3, 8, na 17, ya Umoja wa Mataifa tunafanya juhudi kuleta mabadiliko katika kuzikabili changamoto za afya-msingi katika Nchi za Mapato ya Kiwango cha Chini na Kati. Juhudi zetu zinalenga maeneo yafuatayo:
Chapa ya Impact
Chapa ya toleo la Impact inalenga huduma ya afya kuhusu magonjwa yasiyoambukizwa (NCDs), kama vile ugonjwa wa moyo, saratani, kisukari, katika nchi zilizoteuliwa tunakoendesha shughuli kote duniani.


Changamoo za NCDs
Kila mwaka, watu milioni 17 wanakufa kutokana na NCD kabla ya kufika umri miaka 70 na 86% ya vifo hivi hutokea katika Nchi za Mapato ya Kiwango cha Chini na Kati.1
Je, ni kwa nini tunaona hizi changamoto katika nchi za mapato ya kiwango cha chini na kati?
- Matibabu ya NCD ni marefu na ni ya bei ghali na yanachangia umaskini kutokana na gharama za kiasi kikubwa za kimatibabu na matumizi ya hali ya juu kutoka mfukoni.
- Watu walio katika nchi za mapato ya kiwango cha chini na kati wanao ufikio finyu kwa huduma fanisi za afya na zenye usawa, jambo linalochelewesha ugunduzi wa magonjwa na hatari ya vifo vingi vya mapema.


Jinsi tunavyoshughulikia changamoto hizi
Ili kushughulikia changamoto za NCDs katika nchi zinazokua, Global Health Unit ya Sanofi imebuni suluhisho linaloweza kufikiwa ili kuleta sokoni viwango kadhaa vya huduma za matibabu ya NCD chini chapa ya jina la Impact (INN + Impact).
Kutolewa kwa huduma mbalimbali za Impact na nchi za GHU kutachukua nafasi ya chapa zinazofanana za Sanofi zilizokuweko awali kwa ajili ya magonjwa haya.


Ubora uleule, jina tofauti
Bila kupunguza ubora, jambo la pekee linalobadilika kutoka kwa bidhaa za chapa za Sanofi na kuchukua chapa ya Impact ni jina na ufungaji.
Je, mbona tunabadilisha
Kuzindua Impact badala ya chapa asili ya Sanofi kunatusaidia:
- Kutoa bei za kumudu kwa dawa hizi, hivyo kutoa ubora wa kuwafikia wagonjwa wengi.
- Kutumia kifungio kimoja cha kipekee katika nchi zote katika nchi tunazoendesha shughuli ili kusaidia katika kukinga biashara kinzani
Kwa taarifa zaidi kuhusu badiliko hili, tembelea eneo letu la FAQ

Jon Fairest
Kiongozi wa Global Health Unit, Sanofi
"Tunafanya kazi kuboresha ufikiaji wa dawa muhimu huku tukikuza huduma ya afya yenye thamani bora na endelevu kwa ajili ya watu wa nchi maskini. Ni muhimu kuwa tunafanya kazi na washirika ulimwenguni, kanda na maeneo husika, ili kuleta mabadiliko ya mageuzi na ya kudumu. Kwa kuunda mipango kabambe ya masuala ya afya ambayo imekumbatiwa katika jamii wanazohudumia, tunayo fursa kubwa ya kuboresha huduma na kuunda dunia stahimilivu zaidi"

Jinsi tunavyofanya kazi
Gundua kiini cha tunayofanya ili kushughulikia changamoto za NCDs na kuboresha huduma kwa ajili ya wagonjwa.
Je una swali au unahitaji msaada?
Pata majibu ya maswali ya kila mara katika eneo letu la Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi (FAQ). Labda swali lako limewahi kuulizwa tayari. Ikiwa hutapata jibu lako, unakaribishwa kila mara kuwasiliana nasi.
Marejeleo
- WHO. https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/noncommunicable-diseases, Ilitembelewa mara ya mwisho Julai 2023.
MAT-GLB-2304595 (v5.0) Machi 2025